Kujilinda dhidi ya ulaghai wa uhamiaji
Ulaghai wa uhamiaji wa kujihadhari, na jinsi ya kujilinda dhidi mwenyewe dhidi ya ulaghai huu na udanganyifu wa viza.
Ikiwa unapanga kuomba viza ya kuja New Zealand, kuwa mwangalifu na watu wanaoweza kukulaghai ili waibe pesa zako au kukusajili kwenye kazi ambazo si kama wanazoziahidi.
Hapa chini kuna aina za ulaghai wa kujihadhari na hatua unazoweza kuchukua ili kujilinda dhidi ya ulaghai au udanganyifu wa viza.
Ikiwa tayari unafanya kazi New Zealand na unadhani kwamba unanyonywa au unafanyiwa unyanyasaji kazini, usiogope kuomba msaada kutoka idara ya Uhamiaji New Zealand (INZ). Sisi pamoja na Ajira New Zealand tunaweza kukusaidia na kuchukua hatua ikiwa inahitajika.
Chunguza dalili za ulaghai
Ikiwa unaona dalili hizi za ulaghai, acha kwanza, na uchukue tahadhari za ziada. Uliza maswali na tafuta ushauri rasmi. Unaweza kuzungumza nasi kuhusu wasiwasi wako
Unaombwa kulipia kazi yako
Jihadhari ikiwa unaombwa kuilipia kazi yako ada, wakati mwingine ambazo huitwa ada za “usindikaji” au “uwekaji.”
Waajiri wa New Zealand hawawezi kukutoza ada ili kupata kazi au kukulazimisha kulipa gharama yoyote yao ya uajiri. Hii inajumuisha kupitia mtu wa upande wa tatu ambaye kisha anakuomba kumlipa.
Ikiwa unatumia:
- shirika la ajira, kuwa mwangalifu kuhusu ada zozote za juu ambazo wanataka kukutoza moja kwa moja. Ada zozote kutoka shirika la kuajiri zinapaswa kuendana na huduma wanayokupatia.
- Mshauri wa uhamiaji, utahitaji kulipa ada ya bei inayofaa kwa huduma zao.
Uhamiaji New Zealand tu inakutoza ada ya kuwasilisha ombi. Unaweza kuhitajika kulipa gharama wakati unakusanya ushahidi unaohitajika kwa ombi lako, kama vile kukamilisha uchunguzi wa kimatibabu.
Kupata kipaumbele cha ombi na upatikanaji kwa maafisa wa uhamiaji
Kwa ulaghai huu, mshauri wako, wakala, mshauri mtalaamu au mtu kutoka upande wa tatu wanasema kwamba wanaweza kutumia miunganisho yao ili kuhakikisha matokeo au uamuzi wa haraka.
Huhitajiki kutumia mshauri. Uhamiaji New Zealand:
- haitapa kipaumbele ombi lako kwa sababu unatumia mshauri, na
- inachukua maamuzi tu kwa maombi kwa kutathmini taarifa kulingana na sheria za uhamiaji.
Unaombwa kusema uongo
Ni kinyume cha sheria kusema uongo ili kustahili kupata kazi au viza.
Mshauri wako au mtu kutoka upande wa tatu anavunja sheria ikiwa anakushauri kufanya hivyo. Ni dalili kwamba wanaweza kuvunja sheria zingine za uhamiaji au ajira.
Ni muhimu kwamba taarifa unazozitoa ni za ukweli. Kauli zozote za uongo zitaaathiri maombi yako ya viza ya sasa na baadaye.
Unaambiwa kwamba huna haki za msingi za ajira kama raia wa New Zealand.
Hii si ukweli. Kila mtu huko New Zealand ana haki sawa za msingi, ikiwemo wahamiaji. Hii inajumuisha haki ya kulipwa wakati wa likizo za kazi na za ugonjwa, na haki ya kulalamika kuhusu mazingira ya kazi ambayo si salama.
Watu ambao wanasema kwamba huna haki hizo huenda wanavunja sheria za uhamiaji au ajira.
Haki za msingi za wafanyakazi – Ajira New Zealand
Kuripoti unyonyaji wa mfanyakazi mhamiaji – Ajira New Zealand
Unapewa ofa ya kifurushi chenye malazi
Si kawaida kupewa malazi pamoja na kazi nchini New Zealand.
Ni katika hali chache tu, kama vile kufanya kazi shambani au kwa mtoa huduma ya malazi, ambapo hili linaeleweka.
Kuwa mwangalifu kuhusu ofa za kifurushi chenye viza, kazi na malazi – walaghai wanaweza kujaribu kukutoza kiasi kikubwa cha malazi.
Unaahadiwa makazi
New Zealand inatoa fursa nzuri za kusoma au kufanya kazi. Viza ya muda itakuruhusu kufurahia fursa hizi, lakini hakuna uhakika kwamba zitakufikisha kwa makazi.
Matapeli mara nyingi huzidisha jinsi makazi yanavyoweza kuwa, kwa hivyo kuwa makini kwa sababu hatua za kupata makazi zinahitaji ujuzi, uzoefu, sifa au kazi fulani maalum.
Ahadi kuhusu mapato ya baadaye, ununuzi wa nyumba, au kupata msaada wa serikali.
Unapaswa kuamua kuhamia hapa kulingana na kile unachokipewa, si ahadi za baadaye ambazo huenda zisitimizwe.
Kwa ujumla, huwezi kununua nyumba au kupata msaada wa fedha wa serikali ikiwa huna viza ya makazi. Huwezi kufanya kazi za ziada ili kupata pesa za ziada.
Unaambiwa kwamba unapaswa kutumia mshauri.
Huhitajiki kutumia mshauri ili kuomba viza. Unaweza kuomba viza wewe mwenyewe ukitumia taarifa zilizoko kwenye tovuti yetu.
Ikiwa unaamua kutumia mshauri, ni mshauri wa uhamiaji mwenye leseni (LIA) tu, ambaye ni wakili aliyeidhinishwa wa New Zealand, au mtu mwingine ambaye anaweza kutoa kisheria ushauri wa uhamiaji. Unaweza kuchagua LIA kulingana na lugha yako, eneo na bajeti yako.
Hupati habari za hivi karibuni kuhusu ombi.
Ikiwa mshauri au mtu wa upande wa tatu hakupatii habari za sasa kuhusu ombi lako, unaweza kutembea tovuti yetu ili kujua ni muda gani inachukua kushughulikia maombi.
Ikiwa una wasiwasi kwa sababu hupokei taarifa, unaweza kutuita moja kwa moja ili kuthibitisha hali ya ombi lako.
Inachukua muda gani kushughulikia ombi
Unakutana na barua pepe au tovuti ya kutiliwa shaka inayodai kuwa ya Uhamiaji New Zealand.
Tunafahamu barua pepe au tovuti za kitapeli zinazojifanya kuwa zinatoa huduma za mtandaoni za Uhamiaji New Zealand. Tumia viungo vyetu rasmi kwa huduma hizi ili kuhakikisha kwamba hudanganyiki na kutembelea tovuti bandia. Unaweza kuthibitisha hili kwa kuangalia anuani ya tovuti ili kuhakikisha kwamba ina ndani yake ‘.immigration.govt.nz’ kwa usahihi. Chunguza kwa makini kwa sababu tovuti ya ulaghai inaweza kuonekana sawa.
Anuani rasmi za barua pepe kutoka Uhamiaji New Zealand zinaishia kwa ‘immigration.govt.nz’ au ‘mbie.govt.nz’.
Own your online ni tovuti iliyoundwa Serikali ya New Zealand ili kuwasaidia watu kujifunza mengi kuhusu usalama wa mtandaoni. Ina mwongozo zaidi kuhusu jinsi ya kutambua ulaghai wa mtandaoni.
Pata msaada sasa — Own your online
Unaweza kulipa ada za viza yako au ada za matibabu kwa akaunti ya benki.
Hatutakuomba kamwe kulipi ada za kuwasilisha ombi la viza kwa kuweka fedha kwenye akaunti ya benki. Tunakubali tu malipo kupitia kadi ya benki au ya mkopo kwenye fomu za uombaji za mtandaoni au za karatasi. Unaweza pia kulipia viza yako kwenye Kituo cha Maombi ya Viza kilichoidhinishwa ikiwa uko nje ya New Zealand.
Ofisi Nje ya New Zealand (Vituo vya Maombi ya Viza)
Ni madaktari wa jopo walioidhinishwa tu na madaktari waliosajiliwasajiliwa katika nchi yako ambao wanaweza kukubali malipo kwa matibabu ya uhamiaji. Hatutakuomba kamwe kulipia uchunguzi wa kimatibabu wa uhamiaji. Malipo haya yanapaswa kufanywa kwa kliniki ya jopo la daktari au daktari aliyesajiliwa.
Daktari ambao wanaweza kufanya uchunguzi wa X-ray na wa kimatibabu
Njia za kujilinda dhidi ya ulaghai
- Huhitajiki kutumia mshauri. Ikiwa unachagua kutumia mshauri, mtumie tu mshauri wa uhamiaji mwenye leseni, ambaye ni wakili aliyeidhinishwa wa New Zealand, au mtu mwingine ambaye anaweza kutoa ushauri wa uhamiaji kisheria.
- Ikiwa unachagua kutumia mshauri au shirika la uajiri, ni wazo zuri kulinganisha bei kutoka mashirika au washauri mbalimbali, kwa hivyo unajua kwamba unazilipa huduma zao kwa bei inayofaa.
- Hakikisha kwamba unapata huduma rasmi za mtandaoni za Uhamiaji New Zealand. Angalia kwa umakini tovuti ili kuhakikisha kwamba ina ‘.immigration.govt.nz’ ndani yake kwa usahihi au unapata huduma zetu kupitia tovuti yetu.
- Thibitisha kwamba mwajiri wako mtarajiwa ameidhinishwa. Waajiri wengi wanaoajiri wafanyakazi kwa Viza ya Kazi ya Mwajiri Aliyeidhinishwa anapaswa kuidihinishwa kwanza. Thibitisha kwamba wanatumia zana yetu ya mtandaoni.
Orodha ya waajiri walioidhinishwa
- Zungumza na mwajiri wako mtarajiwa moja kwa moja, kama vile kupitia mahojiano. Kuhama nchi ni uamuzi mkubwa, kwa hivyo kuwa mkweli kuhusu ujuzi wako ili kuhakikisha kwamba unastahili kweli kwa kazi hiyo.
- Ikiwa una mashaka, wasiliana nasi. Tunaweza kukusaidia kujua chaguo zako za viza na iwapo taarifa unayoambiwa na mtu ni sahihi au halisi. Tunaweza kukupa taarifa kuhusu ombi lako. Ikiwa Kiingereza si lugha yako ya kwanza, tunaweza kukuunganisha na mkalimani.
Chaguzi za viza za New Zealand
- Ikiwa unaweza, fanya utafiti zaidi kwa kuwauliza watu kutoka nchi yako ambao wamefanya safari sawa kwenda New Zealand.
Ikiwa mwajiri anatoa malazi, omba picha na uende kwenye tovuti ya Huduma za Upangaji na kulinganisha bei za soko la kodi kwa aina ya mali katika eneo hilo na kujua mengi kuhusu haki zako kama mpangaji.
Linganisha bei za soko la kodi – Huduma za Upangaji
Rasilimami zilizotafsiriwa – Huduma za Upangaji
- Jifunze kuhusu New Zealand, ikiwemo gharama ya maisha na upatikanaji wa huduma ya afya. Tovuti yetu ya Work and Live ina maelezo muhimu.
Kuishi na Kufanya Kazi New Zealand
- Jifunze kuhusu haki zako za ajira kama mfanyakazi wa New Zealand. Tovuti ya Ajira New Zealand ina taarifu muhimu katika lugha nyingi, na moduli ya bure ya kujifunza kuhusu haki za msingi, wajibu na jinsi ya kushughulikia matatizo ya ajira.
Haki na wajibu wa mfanyakazi – Ajira New Zealand
- Matapeli wakati mwingine wanatoa viza bandia. Ikiwa wakili au mshauri amesema kwamba umeisha pewa viza ya New Zealand, unaweza kuthibitisha ikiwa ni ya kweli kwa kutumia huduma yetu ya Uthibitishaji wa Viza.
Huduma ya Uthibitishaji wa Viza
- Ripoti ulaghai kwa viongozi wa eneo lako katika nchi yako kama vile Polisi. Ikiwa uko nchini New Zealand, unaweza kuuripoti mtandaoni ulaghai kwa tovuti ya Own your website.
Pata msaada sasa — Own your online
Rasilimali kwa mashirika yanayofanya kazi na wahamiaji
Ikiwa unafanya kazi na watu wanaopanga kusoma, kufanya kazi au kuishi nchi New Zealand, kutumia kifurushi chetu cha mitandao ya kijamii ili kuwasaidia kutambua uwezekano wa ulaghai au udanganyifu wa uhamiaji.
Rasilimali hizi zinapatikana katika Kiingereza na lugha zingine.
Vifurushi vya mitandao ya kijamii vya ulinzi dhidi ya ulaghai wa uhamiaji